
WANYAMA WA KUSHANGAZA WANAOISHI BAADA YA "KUFA" !!!
WANYAMA WA KUSHANGAZA WANAOISHI BAADA YA "KUFA" !!!
Labda umegundua kuwa, miili ya binadamu hufanya kazi vizuri na mifumo yetu ya neva na akili zetu, viungo vetu pamoja na viungo vikuu vyote vimeunganishwa na kuwasiliana kufanya majukumu yao ipasavyo.
Nahisi kua leo ni jukumu langu kukujuza kwamba sio viumbe wote wameunganishwa kwa namna hii kama binadamu . ndo mana leo ntakujuza kuhusu Viumbe usiojua kuwa wanaeza kuishi kwa muda ata baada ya miili yao kutenganishwa
Mnyama wa wa kwanza atakua ni
1: Nyoka
Unapokabiliwa na nyoka mwenye sumu, athari ya asili inaweza kuangukia moja ya aina tatu: kukimbia, kushtuka na kusimama papo hapo au hata kuamua kumuua kwa kukata kichwa chake
Umeonywa kuto mkata nyoka shingoni, Maamuzi ya kumkata kichwa na kumuua yanaweza kuonekana kua ndio suluhisho kamili la kukabiliana na nyoka huyu , ila fahamu kwamba jambo hili linaweza kuvuruga kila kitu na kusababisha madhara makubwa.
Nyoka ana shimo kwenye pande za uso wake, ambazo hutumia kugundua vitisho - ikiwa upo karibu na joto la mwili wako kugundulika, basi jua kwamba upo karibu Zaidi kuonekana kama tisho kwani kichwa cha nyoka bado kinaweza kumngata mtu baada ya kukatwa na kutenganishwa na mwili .kinaishi pia kwa muda
2: Mende
Hivi wajua kwamba Mende ni maarufu kwa uimara wao, na mara nyingi hutajwa kama manusura, katika vita vya kinyuklia. Ila amini usiamini , utafiti umebaini kweli kwamba mende ni mdudu anayeweza kuishi wiki kadhaa hata baada ya kukatwa kichwa chake.
3:Kuku
Kama ushawahi kumchinja kuku basi utakubaliana name kua Ukikikata kichwa cha kuku, bado anaweza kuzunguka kwa sekunde chache. Wanyama kadha wa kadha wa uwezo wa kufanya hivyo kwa sababu mtandao wa neural kwenye kamba za uti wa mgongo zimepangwa ili kuweza kuelekeza misuli katika mifumo anuwai ya mara kwa mara ya harakati kama vile kukimbia. Licha ya utafiti wa kina juu ya jinsi mwili, ubongo na mfumo wa neva unavyofanya kazi, wanasayansi bado hawajapata picha kamili ya jinsi seli za ujasiri zinavyowasiliana kufanya harakati kama hizi .
4: Octopus au pweza
Imegunduliwa na kudhibitishwa kwamba Mahema ya pweza almaarufu kama tentacles ambayo ni mikono inayotumika kuokota chakula na wanyama hawa wa majini , bado hua hai saa moja baada ya kukatwa kutoka kwa mmiliki wao aliyekufa, na hata hujaribu kuokota chakula .
5: Minyoo
Hadithi ya minyoo ni simulizi ambayo inaumaarufu kote : ikiwa utamkata minyoo katikatikati, basi ni kweli kuwa mwili utatengana , ila watakua minyoo wawili waliohai .cha kushangaza Zaidi kua ukikata sehemu yoyote ya mwili wake , basi kua tayari kushuhudia miujiza baada ya siku kadhaa kwani kiungo ulichokata utapata kimemea tena baada ya siku kadhaa .
6: Vyura
Shukrani kwa mwana sayansi david ferria .katika karne ya kumi na tisa , mwanasayansi huyu alishawishi wenzake waondoe ubongo wa chura, ili waone kitakachotokea. Waliishia kubaini kuwa chura mwenye kichwa bila ubongo , anaishi sawa tu na chura mwenye kichwa na ubongo wake Ukimgeuza, atageuka na kusimama sawa; ukimfinya miguu yake, ataruka; ukimtumbukiza ndani ya maji , ataogelea upande na kujaribu kutoka kwenye maji na labda ,kinachotisha Zaidi ni kuwa ataishi tu maisha yake ya kawaida kama chura mwenye ubongo.
7:Nzi wa maua
Nzi wa kike wa maua , wataishi kwa siku kadhaa baada ya kichwa chao kutenganishwa na mwili. Nzi hawa huchukua msimamo ulio sawa na ule wa nzi wa kawaida wanaweza kuruka na pia kutembea bila tatizo lolote.
8: Kobe wa maijini
Ukikata kichwa cha kobe wa majini , bado anaweza kuogelea. Mfumo wa mwili wa kobe umeumbwa kumsaidia kuogelea, mtandao wa neural kwenye mgongo umepangwa vyema kusaidia katika harakati za kuogelea hata bila ya kobe mwenyewe kuwa na kichwa .
9:salamander
Je wajua kua miguu ya salamander inaweza kuzaliwa au kua upya ata baada ya kukatwa?
Ni kweli. ila kulingana na utafiti, uwezo wao kufanya hivi hutegemea mfumo wao wa kinga
Utafiti wa axolotl, ambaye ni salamander wa majini, unaonyesha kwamba seli za kinga zinazoitwa macrophage ni muhimu katika hatua za mwanzo za kuunda tena viungo vilivyopotea. Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha mikakati inayowezekana ya ukarabati wa tishu kwa wanadamu.
PRESENTER ALI: Channel maalumu ya Burudani na EXCLUSIVE interview kutoka kwa mastaa Hakikisha unaSubscribe .
SHUKRAN Ni follow kwenye mitandao ya kijamii.
INSTAGRAM : http://www.instagram.com/presenterali
TWITTER : http://www.twitter.com/presenterali
FACEBOOK:http://www.facebook.com/presenterali1
KWA MATANGAZO
PIGA : +254704589139
BARUA PEPE : [email protected]
