
Huu Ndio UHALISIA Katika ASILI......Kama HUJAJIFUNZA basi UMEKOSA SOMO MUHIMU SANA 😭😭
#ufugaji #africa #biashara
Umejifunza nini kutoka katika Asili Leo ?
Kama hutumii ASILI kujifunza basi unakosa masomo mengi sana kwani hata wabunifu wote wazuri hutumia ndege, wanyama, mimea n.k ili kufanya ubunifu wao.
Mara kadhaa rangi za nguo ni matokeo ya ubunifu wa kusoma rangi za ndege/wanyama au mimea.
Wagunduzi wa vifaa na teknolojia mbalimbali waliisoma kwanza asili! Wakatengeneza ndege ipaayo kwa kutumia ndege apumuaye! Meli ilitengenezwa kwa kumsoma samaki n.k.
Unadhani ni kwa nini wavumbuzi sasa wanatumia kila gharama kwenda mwezini na hata kwenye sayari ya Mars?
